Rais Samia atoa wito kwa wawekezaji viwanda vya sukari

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wawekezaji katika viwanda vya sukari nchini kuchangia kikamilifu kufanikisha malengo ya kujitosheleza. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera leo Juni 9, 2022, anaendelea na ziara yake ambayo ni siku ya pili mkoani humo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi. 

Mheshimiwa Rais Samia amesema hayo leo alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Missenyi mkoani humo na kutaka tufikie ziada ya kuuza nchi za nje ifikapo 2025. 

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imeazimia kufanya mageuzi ya kilimo cha kisasa ambayo yanapaswa kwenda sambamba na mahitaji ya viwanda vya ndani ili kuifanya nchi iweze kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo Afrika. 

Katika kutekeleza mageuzi hayo, Rais Samia amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha alizeti na michikichi mkoani humo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa kuzalisha Umeme Megawati 20 katika Kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera leo Juni 9, 2022.

Rais Samia amesema, lengo la kuanzisha kilimo cha mazao hayo ni kuzalisha mafuta ya kujitosheleza ndani ya nchi, kuwawezesha vijana kujiajiri na kuinua uchumi wa Mkoa huo. 

Vile vile, Rais Samia amewataka wawekezaji kuiga mfano wa Mwekezaji wa kiwanda cha Kagera Sugar kwa kuajiri vijana katika shughuli muhimu za kilimo ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali vya hapa nchini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Udege kuhusu uandaaji na uchakataji wa miwa wakati alipotembelea kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo mkoani Kagera leo.

Aidha, Rais Samia amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kurekebisha Sera, Sheria na Kanuni zitakazochochea uwekezaji endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news