Jaji Mdemu:Taaluma hii iwaongoze kutekeleza Dira ya Mahakama

NA INNOCENT KANSHA-Mahakama

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu amewasisitiza Wahasibu na Wakaguzi wa ndani kutumia taaluma, maadili, miongozo, sera na sheria kurahisisha utelelezaji wa dira ya Mahakama inayohusu Upatikanaji wa Haki kwa Wakati na kwa Wote.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akiwa kwenye picha na kundi la Wahasibu wanaoshiriki mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni, 2020, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wapili kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manote (wa kwanza kushoto), Afisa Mkaguzi Mahakama ya Tanzania, Bw. John Ramadhan (wa pili kushoto) na Afisa Utumishi Mahakama ya Tanzania, Bw. Rajabu Singana (wa kwanza kulia).
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akifafanua jambo kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wakati wa kufungua mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani, leo tarehe 13 Juni, 2022.
Sehemu ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wakiwa kwanye Ukumbu wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma wakifuatilia mtoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wakiwa kwanye Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma wakifuatilia mtoa mada wakati wa mafunzo hayo.

Akifunga mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani yatakayofanyika kwa siku tano katika Ukumbu wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni 2022 Jaji Mdemu amesema, dira hiyo haiwezi kutekelezeka iwapo mifumo ya kihasibu waliyojifunza haitaondoa usumbufu kwa wadaawa kufanya malipo mbalimbali ya usajili wa mashauri na nyaraka za kimahakama kwa ufanisi, kulipa mirathi kwa wakati na watumishi wa ndani kulipwa stahiki zao bila usumbufu na kucheleweshwa.

“Pengine jambo la msingi ambalo mnatakiwa kulifahamu na kupitia mafunzo haya mtalifahamu ni kuwa upatikanaji wa haki kwa wakati na kwa wote haliwahusu maafisa wa Mahakama tu, bali hata ninyi mnahusika kwa asilimia mia moja katika utoaji wa huduma ya haki unaomlenga mwananchi na hivyo tukakatimize kwa vitendo,”aliongeza Jaji Mdemu.

Mhe. Mdemu akatoa rai kwa Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani kutumia ujuzi mtakaoupata katika mafunzo hayo kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutatua changamoto za utoaji wa huduma za kihasibu ili kurahisisha na kuondoa usumbufu kwa wadaawa mnaowapa huduma, kwani TEHAMA ndiyo msingi wa kurahisisha upatikanaji wa huduma, kwa kuwa ninyi ndo mmefunzwa kuhusu matumizi ya hiyo mifumo basi msiende kuwa msiwe kikwazo cha utoaji huduma bora kwa wadaawa.

"Mahakama ya Tanzania inanuwia kuwa na maamuzi bora ya kimahakama ambapo imejiwekea malengo ya kukuza uelewa wa misingi ya taaluma ya kisheria na kuongeza ujuzi kwa watumishi wa mahakama. Katika kutekeleza malengo hayo, Mahakama imejiwekea mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama wa ngazi zote. Mmejengewa uwezo kwenye eneo lenu la kihasibu. Sasa hakutakuwa na kisingizio cha kuchelewesha huduma, hususani masuala ya mirathi ambayo yanahitimisha maamuzi yanayotolewa na Mahakimu na Majaji,"'liongeza Jaji Mfawidhi.
Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (aliyesimama mbele kulia) akielezea jambo wakati wa mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wakiwa kwanye Ukumbu wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akiwa kwenye picha na kundi la Wakaguzi wa Ndani wanaoshiriki mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni, 2020, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wapili kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manote (wa kwanza kushoto), Afisa Mkaguzi Mahakama ya Tanzania, Bw. John Ramadhan (wa pili kushoto) na Afisa Utumishi Mahakama ya Tanzania, Bw. Rajabu Singana (wa kwanza kulia).
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akiwa kwenye picha na kundi la Wahasibu wasaidizi wanaoshiriki mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni, 2020, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wapili kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manote (wa kwanza kushoto), Afisa Mkaguzi Mahakama ya Tanzania, Bw. John Ramadhan (wa pili kushoto) na Afisa Utumishi Mahakama ya Tanzania, Bw. Rajabu Singana (wa kwanza kulia).
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akiwa kwenye picha na Sekretariati kwenye mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni, 2020, wengine ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Bernard Mpepo (wapili kulia), Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manote (wa kwanza kushoto), Afisa Mkaguzi Mahakama ya Tanzania, Bw. John Ramadhan (wa pili kushoto) na Afisa Utumishi Mahakama ya Tanzania, Bw. Rajabu Singana (wa kwanza kulia).(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)

Kuhusu mada zilizofundishwa Jaji Mdemu alisema maeneo yote yaliyofundishwa na wawezeshaji ni muhimu sana na yanahusu utekelezaji wa majukumu yao kama Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani kitaaluma na kimaadili. "Mmepewa nyenzo muhimu za utekelezaji kwenye maeneo mengine yaliyo nje ya taaluma yenu lakini hayaepukiki katika kuhakikisha mnatimiza wajibu wenu katika kutoa huduma ya kihasibu. Mlikuwa na majadiliano mbalimbali ambayo yaliwawezesha kubadilishana uzoefu katika kazi zenu, mkayatumie yote mliyoyapata katika kufanyia kazi", alisema Jaji Mdemu.

Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama 2020/2021-2024/2025 ambapo katika Tunu ya Tano kuhusu weledi, Mahakama itatekeleza majukumu ya utoaji haki kwa umahiri na ufanisi. Aidha, ndani ya Mpango Mkakati huo, katika nguzo ya kwanza inayohusu utawala, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, moja ya lengo ni kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi zote.

Post a Comment

0 Comments