CCM Vingunguti yaanza kutoa fomu za kuwania uongozi

NA DIRAMAKINI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam kinawatangazia wanachama wote kuwa fomu za kugombea Uongozi wa CCM ngazi ya Kata zimeanza kutolewa leo tarehe 13/06/2022 hadi tarehe 20/06/2022, muda ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, nafasi zinazogombewa ni:
1. UENYEKITI WA CCM KATA nafasi moja.

2. UKATIBU WA CCM KATA nafasi moja.

3. UKATIBU WA SIASA NA UENEZI KATA nafasi moja.

4. UJUMBE WA H/KUU KATA nafasi tano.

5. UJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA nafasi tano.

6. UJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA nafasi moja.

Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi Kata ya Vingunguti.

Post a Comment

0 Comments