Mchina atuhumiwa kumuua mwenzake Dar

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamtafuta mtuhumiwa, Zheng Lingyao (42) raia wa China mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26) raia wa China, mfanyabishara na mkazi wa Kalenga Ilala jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Muliro Jumanne ambaye ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

"Tukio hilo limetokea Juni 11,2022 Mtaa wa Kalenga Ilala kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku ambapo Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqin (32) Raia wa China na badaye alimfyatulia risasi FU, raia wa China ambaye alipoteza maisha.

"Nie anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili, uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi," amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news