Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Juni 13,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.09 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.77 na kuuzwa kwa shilingi 11.42.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Juni 13, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Dola ya Singapore (SGD) inanunuliwa kwa shilingi 1662.6 na kuuzwa kwa shilingi 1668.8 huku Krona ya Sweden (SEK) ikinunuliwa kwa shilingi 228.6 na kuuzwa kwa shilingi 230.80. 
Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 145.33 na kuuzwa kwa shilingi 146.03 huku dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2290.36 na kuuzwa kwa shilingi 2313.26.

Dinar ya Algeria (DZD) inanunuliwa kwa shilingi 16.53 na kuuzwa kwa shilingi 16.54 huku Franka ya Ufaransa (FRF) ikinunuliwa kwa shilingi 308.31 na kuuzwa 311.04.

Lira ya Italia (ITL) inanunuliwa kwa shilingi 1.044 na kuuzwa kwa shilingi 1.054 huku Rupia ya India (INR) ikinunuliwa kwa shilingi 29.33 na kuuzwa kwa shilingi 29.61.

Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.59 na kuuzwa kwa shilingi 19.75 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2410.14 na kuuzwa kwa shilingi 2434.47.

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.63 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.13 na kuuzwa kwa shilingi 50.58.

Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.79 na kuuzwa kwa shilingi 1.80 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7482.4 na kuuzwa kwa shilingi 7542.4

Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 343.8 na kuuzwa kwa shilingi 347.26 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.06 na kuuzwa kwa shilingi 17.24.

Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 623.67 na kuuzwa kwa shilingi 629.7 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 146.9 na kuuzwa kwa shilingi 148.3.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news