Miaka yangu mitatu ya kikazi Ngorongoro, tatizo ni kundi moja kutoheshimu mipaka ya mwingine

NA CHIOMA MAZIKU

SINA interest (maslahi) yoyote na yanayoendelea huko Ngorongoro ila nimeishi kama mfanyakazi ndani ya Ngorongoro kwa miaka mitatu (2010-2013). Ngorongoro ina taarafa tatu;

1) Loliondo

2) Ngorongoro

3) Sare

Taarafa moja ya Loliondo ndio kuna vijiji kama Waso, Loliondo na vingine vingi huku tarafa mbili Ngorongoro ndio inabeba mpaka Crater yenyewe na vijiji vingine vingi.
Taarafa ya tatu ya Sare. Yenye ndio ilikuwa anapatikana Babu wa Samunge, hii ina vijiji vingi sana.

Wakazi wa taarafa mbili za Loliondo na Ngorongoro asilimia kubwa zinakaliwa na jamii ya Wamasai na Wakazi wa Taarafa ya Sare asilimia kubwa ni Wasonjo.

Japo katika Taarafa ya Loliondo Mjini kwao kuna mchanganyiko wa Wasonjo kidogo na Wamasai.
Wakati naishi huko, hao jamaa ilikuwa hauishi mwaka bila vita ya Wamasai na Wasonjo. Na ilikuwa noma kinoma,Tarafa ya Sare yenyewe haina shughuli nyingi za kitalii na ndio maana katika heka heka hizi zinazoendelea kusikii wakitajwa.

Tarafa ya Ngorongoro ndio Baba Lao kwa utalii kutokana na uwepo wa Crater. Sheria za kuishi EneolLa Hifadhi ni ngumu na shughuli nyingi zimezuiwa kufanyika Tarafa ya Ngorongoro.
 
Utalii upo kwa sababu kuna maeneo yana vitalu vya watu kwa ajili ya utalii kama Thompson Safari, Frankfurt na Wengineo akiwemo Mwarabu.
 
Wakati nipo kule hii migogoro ya Wamasai na hawa wawekezaji kwenye hivi vitalu Ilikuwa ni ya mara kwa mara sana. Si unajua Masai huwa haletewi utani linapokuja suala la ng'ombe wake kupata malisho? Huwa hataki na haangalii kama ataharibu mali yako au la!.

Kwa hiyo, hapo ndio tatizo linapoanzia, Mwenye Kitalu anawaza wanyama wake watahama kwa kukosa malisho maana Masai hanaga ng'ombe wawili au watatu na Masai anawaza ng'ombe wake watakufa kama utamzuia kuingia kwenye malisho ili ng'ombe wake washibe.
Basi wenye vitalu hukimbilia Serikalini kuomba suluhu kwa maana wao ndio mabosi. Always Serikali husimama na Mwekezaji ili waendelee kupata kodi yao, hivyo huamua kuwaita mezani kati ya mwekezaji na Wamasai.

Na maamuzi ya mwisho huwa ni kuwekeana mipaka ambayo wanakubaliana kila mtu anashika lake.

Tatizo linakuja kuibuka Tena 

Masai wakati wa kulisha huingia mpaka kwa Mwekezaji, ndio vita inapoibuka na Masai hakubali ng'ombe wafe njaa wakati majani anayaona lazima atawaswaga waje kula, kinachoendelea Loliondo ni mgogoro wa kimipaka.
 
Ambao hapa ndipo mambo yanapochanganywa kutofautishwa kati ya kundi linalotakiwa kuhama na kati ya kundi lilotakiwa kuheshimu mipaka ya mwenzake.Ndio imefikia hatua ya kuwekwa Bikoni watu wameandamana.

Post a Comment

0 Comments