Milioni 154.9/- zachangishwa kuondoa uhaba wa madawati shule za msingi Ilemela

NA SAMIR SALUM (Langolahabari)

JUMLA ya Shilingi Milioni 154,910,000 zimechangiwa kwa ajili ya kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati katika shule za msingi zilizopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akitoa neno akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla (Kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Veronica Kessy Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Johari Musa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kali katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022. (Picha Zote na Samir Salum, Lango La Habari).


Fedha hizo zimechangwa usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022 katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka kwa usimamizi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Hassan Masalla na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula.

Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla kwa kuwa na maono na kuelekeza jitihada katika kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati kwenye shule za msingi.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwa ni Mgeni Rasmi katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akizungumza katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.“licha ya kuwa Serikali italeta mpango katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo ila hatuwezi jua utaelekezwa sehemu ipi inaweza kuwa maabara, hostel au kwa ajili ya walimu..nikupongeze Mh Dc kwa kuja na mpango wa madawati kwa shule za Msingi” Amesema Dkt. Mabula

Dkt. Mabula amewaasa wadau mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inashirikiana na wadau hao huku akichangia jumla ya madawati 340.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla amesema kuwa Mwaka jana serikali kupitia Rais wa Jamhuri wa Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitoa Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Tisa kupitia Fedha za Uviko-19 kwa ajili ya kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa katika Wilaya ya Ilemela ambapo imeondoa changamoto ya upungufu wa madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.Dc Masalla amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni upungufu wa madawati katika shule za msingi zilizopo Wilayani Ilemela ambapo jumla ya madawati 5830 yanahitajika.

Amesema kabla ya kuwaita wadau kwa ajili ya kuchangia Wilaya kupitia Manispaa yake imetoa fedha za kumalizia majengo ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi, kuongeza shule katika wilaya na kuongeza madawati 1000.

“Uandikishaji wa shule ya Msingi umekuwa maradufu hali inayopelekea kuleta changamoto ya upungufu wa madawati ambapo katika darasa moja linalopaswa kuwa na wanafunzi 45 utakuta zaidi ya wanafunzi 150, tulihitaji madawati 6830 ila sisi kupitia Manispaa yetu tumetoa Madawati 1000 hivyo yamesalia madawati 5830” amesema DC Masalla.

Aidha amewashukuru wadau wote waliochangia katika hafla hiyo ambayo jumla ya shilingi 154,910,000 zilipatikana huku akiwaalika kushiriki siku ya kukabidhi madawati hayo itakayofanyika Julai Mosi, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewaasa wakuu wa wilaya na viongozi wengine katika ngazi zao kuiga mfano wa Dc Masalla hali itakayosaidia kupunguza changamoto huku akichangia shilingi milioni moja.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwa na katibu wa Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula (Kulia) akiteta Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Johari Musa katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.
Baadhi ya wadau wakichangia fedha katika Hafla ya chakula cha hisani kuchangia Madawati ya Shule za Msingi Wilaya ya Ilemela iliyofanyika katika ukumbi wa Winterfall Nyasaka usiku wa kuamkia leo Juni Mosi, 2022.

“Nampongeza kwa maono yake na ubunifu wake mkubwa kwa kuona pamoja na mapato yetu ya ndani na changamoto za Wilaya umeamua kuanza kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata madawati, huu ni ufunguo kwa wakuu wa wilaya wengine kuleta ubunifu kama huu ili kuondoa changamoto za nchi,”amesema RC Mhandisi Gabriel.

Wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za Fedha,Taasisi Binafsi,Wawekezaji, Mahotel,Mashirika na watu binafsi wameshiriki katika kuchangia Fedha kwa ajili ya kupunguza ama kuondoa kabisa Adha ya upungufu wa madawati katika Shule za Msingi zilizopo Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

Post a Comment

0 Comments