Mkurugenzi Mkuu TPA ateta na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika kubwa la meli duniani

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi leo amekutana na kufanya Mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa shirika kubwa la Meli la Linear Messina duniani lenye makao makuu nchini Italia,Ignazo Messina katika ofisi za Bandari jijini Dar es Salaam.

Katika ugeni huo Mkurugenzi wa Messina amemkabidhi tuzo ya ushirikiano mzuri baina ya TPA na Messina.

Ignazo amefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa TPA na ameahidi kushirikiana zaidi na TPA Messina ili kuongeza idadi ya meli zitakozoingia bandari za Tanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TPA ,Eric Hamissi ameahidi kuongeza ushirikiano mzuri na shirika hilo ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia meli zinazoingia katika Bandari ya Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments