Mwanafunzi wa miaka saba akutwa ameuawa kwa kuzibwa mdomo na chandarua wakati akibakwa na kijana wa miaka 40 mkoani Pwani

NA DIRAMAKINI

MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka saba ameuawa kwa kuzibwa mdomo na chandarua wakati akibakwa na kijana ambaye jina lake limehifadhiwa.

Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (40) alimfanyia kitendo hicho cha unyama mwanafunzi huyo wa darasa la pili Shule ya Msingi Misugusugu.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo imesema kuwa, mtuhumiwa alitendea tukio hilo nyumbani kwake.

Amesema kuwa, tukio hilo limetokea Mei 30,mwaka huu huko mtaa wa Vitendo Misugusugu Kata ya Misugusugu wilayani Kibaha ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka.

Lutumo amesema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo la mauaji wakati akimbaka mwanafunzi huyo ambapo aliziba mdomo kwa kutumia chandarua ili asipige kelele na kusapabisha kifo hicho.

Aidha, amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwafuatilia watoto wao na kuzungumza nao mara kwa mara juu ya kujilinda wenyewe ka kutoa taarifa za haraka juu ya wanaowasumbua.

Post a Comment

0 Comments