SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022: Kutambua mahitaji, mwanzo wa kuhudumiwa,tujiandae

NA LWAGA MWAMBANDE (KiMPAB)

AGOSTI 23, 2022 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo ina sura tofauti ikilinganishwa na sensa zilizopita.

Mosi, sensa hii inatarajiwa kuwa na mafanikio kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na pili itafanyika kwa mfumo wa kisasa kupitia vishikwambi.

Lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi kwa wakati kutoka kwa kila mtu ambaye amelala ndani ya mipaka ya Tanzania usiku wa kuamkia sensa hiyo.

Kwa upekee, mshairi wa kisasa Bw.Lwaga Mwambande ambaye anasema tayari amejiandaa kuhesabiwa na familia yake yote, anatumia kalamu yake kukushirikisha mambo muhimu kupitia shairi. Karibu;

1:Ni muda kujiandaa, upate kuhesabiwa,
Usikate washangaa, kama vile wajibika,
Popote pale waka, ujue utafikiwa,
Sensa ya taifa letu, kwa maendeleo yetu.

2:Agosti shinatatu, Siku ya kuhesabiwa,
Tena kwa wote watatu, maswali yatajibiwa,
Binadamu sote watu, tupate kutambuliwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

3:Faida nyingi za sensa, subiri utaambiwa,
Afya Bora ya kisasa, huduma utapatiwa,
Elimu hatutakosa, watoto watapatiwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

4:Kutambua mahitaji, mwanzo wa kuhudumiwa,
Takwimu ndio mtaji, Turkish kuhesabiwa,
Mipango tunahitaji,vizuri tutapangiwa.
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

4:Huduma za maji Bora, tuweze tukapatiwa,
Kuhesabiwa ni sera, idadi kuelewa,
Tutapata bila kura, kama tutahesabiwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

5:Barabara zetu hizi, ili tuweze jengewa,
Tuyajue matumizi, kwa jinsi zitatumiwa,
Hapo bila ya ajizi, ujanja kuhesabiwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

6:Umeme kweli muhimu,haupaswi jadiliwa,
Kila mtu ana hamu, aweze akafikiwa,
Bila takwimu vigumu, kila mtu kufikia,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

7:Shime wote wananchi, muhimu kuhesabiwa,
Tujinue hii nchi, idadi imefikiwa,
Hata shule za makenchi, nazo tuweze jengewa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

8:Sote tukihesabiwa, takwimu kuchukuliwa,
Hapo twahakikishiwa, huduma tukipatiwa,
Zaweza kutosha sawa, bila ya kupungukiwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.

9:Sensa watu na makazi, uende kuhesabiwa,
Huo ndio mwanzo wazi, mipango kufanikiwa,
Watoto hata wazazi, muhimu kuhesabiwa,
Sensa ya taifa letu,kwa maendeleo yetu.
 
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmaill.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news