NBS yakoleza kasi ya uelimishaji kuhusu Sensa, viongozi wa dini Lindi na Mtwara wafikiwa

NA MWANDISHI WETU

VIONGONZI wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara wamesema wananchi wa maeneo yao wapo tayari kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022.
Wakizungumza kwenye Mkutano uliojumuisha Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wamesema Sensa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo hasa kwa wananchi wanao waongoza.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe. Anne Makinda amesema viongozi wa Dini ni nguzo muhimu katika kufanikisha Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha waumini wao kufahamu umuhimu wa Sensa na faida zake ili waweze kushiriki kikamilifu.

Mhe. Makinda ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu ya Sensa kila wanapokutana na waumini wao ili waumini watambue ushiriki wao kwenye Sensa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema, Mkoa wa Mtwara unaendelea vizuri na maandalizi ya Sensa na wananchi wapo tayari kuhesabiwa kwa ajili ya kupata takwimu zitakazotumika kwenye kupanga mipango ya maendeleo.

“Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news