OR-TAMISEMI yaridhishwa na ujenzi wa miundombinu Kituo cha Afya Hoteli Tatu

NA OR-TAMISEMI

TIMU ya Usimamizi Shirikishi kutoka Idara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seali za Mitaa(OR-TAMISEMI) imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ya Kituo cha Afya Hoteli Tatu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Kituo cha afya Hoteli Tatu kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Aidha, timu hiyo imetoa rai kwa Kamati ya Usimamizi wa Shughuli za Afya (CHMT) Halmashauri ya Kilwa kuendelea kuzingatia ubora wakati wa utekelezaji ili miundombinu hiyo idumu kwa muda mrefu lakini pia kuepusha adha na gharama ya kufanya ukarabati wa miundombinu mara kwa mara.
Timu ya usimamizi shirikishi kutoka OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Usimamizi wa shughuli za Afya (CHMT) Halmashauri ya Kilwa ikikagua ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu Juni 2,2022.

Hayo yamebainishwa Juni 2,2022 na Bw. Mathew Mganga Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dawa Ofisi ya Rais-TAMISEMI alipozungumza kwa niaba ya timu hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa shughuli za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

“Ujenzi upo katika hatua nzuri, ubora na viwango unaridhisha lakini tuendelee kuzingatia ubora ili miundombinu hii idumu kwa muda mrefu lakini Pia kuondokana na adha ya kufanya ukarabati mara kwa mara” Bw. Mganga
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za dawa kutoka Idara ya Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Mathew Mganga ( wa pili kushoto) akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Kilwa Juni ,2, 2022 wakati timu ya usimamizi shirikishi kutoka OR-TAMISEMI ilipotembelea hospitali hiyo kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa shughuli za afya.

Kwa upande mwingine timu hiyo imewataka wajumbe wa CHMT kuhahakikisha wanaimarisha usimamizi na ufatiliaji katika ujenzi wa Jengo la dharula linaloendea kujengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati ifikapo tarehe 30 juni 2022.

Sambamba na hilo Bw. Mganga ametoa wito kwa wajumbe wa CHMT kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi pamoja na kushiriki kikamilifu katika zoezi la ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kuleta uelewa wa pamoja lakini pia kuwa na taarifa sahihi za utekelezaji wa shughuli za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news