RC Kafulila: Ole wake atakayechezea maslahi ya mkulima wa pamba Simiyu

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Simiyu,Mheshimiwa David Kafulila amesema,hatawafumbia macho wanunuzi wa pamba au mtu yeyote ambaye atabainika kuwaibia wakulima kupitia mizani feki katika zoezi la ununuzi wa zao hilo linaloendelea kwa sasa.
"Kila atakayehusishwa au atakayebainika kweli anahusika na udanganyifu fulani,iwe wa kucheza na mzani,kwamba mzani wake upo sawa sawa.
"Iwe kwa kumdanganya mkulima kwa namna yoyote ile...awe mtu wa ushirika, awe afisa afisa wa serikali au mtendaji wa Serikali, awe mteule yoyote, awe kiongozi yoyote akihusishwa na jambo fulani, ambalo ni kucheza na maslahi ya mkulima, ama kucheza na wizi, maana yake huyo nitaagiza akamatwe awe ndani na hatua zichukuliwe". 

Post a Comment

0 Comments