Rhobi Samwelly:Watanzania asiwepo mtu yeyote atakayeachwa bila kuhesabiwa Agosti 23

NA FRESHA KINASA

MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT), Rhobi Samwelly ametoa rai kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu. Ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo. 
Kutokana na umuhimu wa Sensa kwa maendeo ya nchi na watanzania, Rhobi akiwa barani Ulaya ameieleza DIRAMAKINI kuwa,Watanzania wote wana wajibu wa kuhesabiwa katika kuiwezesha serikali kupata takwimu sahihi ambazo itazitumia kupanga mipango ikiwemo ya afya, uchumi, miundombinu, elimu, huduma za jamii na kupeleka maendeleo kwa wananchi kwa manufaa yao,jamii na taifa kwa ujumla. 

"Asiwepo mtu yeyote atakayeachwa bila kuhesabiwa Agosti 23, mwaka huu. Serikali ina dhamira njema sana ya kuendelea kufikisha Maendeleo kwa wananchi, ili izidi kufanikiwa zaidi lazima iwatambue Watanzania wote. Hivyo sensa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu,"amesema Rhobi. 
"Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa Serikali wameendelea kutoa msisitizo juu ya mwitikio chanya wa kila mtanzania kuhesabiwa siku hiyo. Naomba Watanzania kuzingatia maelekezo hayo muhimu kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi liweze kuwa na ufanisi mkubwa kwa ustawi wa nchi yetu," amesema. 

Pia, Rhobi amewaomba viongozi wa dini, na wenye nafasi mbalimbali katika jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao juu ya umuhimu wa sensa, kwani jambo hilo ni Muhimu sana lazima liendelee kuzungumzwa mara kwa mara, kusudi siku ikifika Watanzania wote wahesabiwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news