Sensa itakuwa safi kwangu, nipo makazi bora asema mmoja wa wakazi wa Ngorongoro aliyeamua kuondoka kwa hiyari kwenda Msomera


"Ninajisikia fahari kwamba, nimeondoka eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa hiyari yangu kuja Kijiji cha Msomera, Handeni jijini Tanga, ni fahari kubwa kwangu kwa sababu sasa nitaishi maisha mapya, yenye makazi bora ambayo yanaongeza hadhi na heshima yangu kama mfugaji,hii itaniwia rahisi hata wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23 nami niweze kuingizwa kwenye kumbukumbu ya watu wanaomiliki makazi bora, kwa kweli nilichoka na wengi wetu tulichoka kuishi maisha duni, licha ya kujaliwa mifugo ya kutosha tunaishi katika maboma, hii ni ajabu mno. Hivyo ndugu mwandishi, nimejiandaa kuhesabiwa nikiwa makazi yangu ya kisasa hapa Msomera,"ameeleza mmoja wa wakazi wa Ngorongoro ambao wameamua kuondoka kwa hiyari yao katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha na kwenda kuishi Kijiji cha Msomera mkoani Tanga. (Mazungumzo na DIRAMAKINI leo Juni 20,2022).

Post a Comment

0 Comments