Serikali yapunguza tozo ya ving’amuzi nchini

NA DIRAMAKINI

SERIKALI imepunguza tozo ya ving’amuzi nchini kufikia shilingi 500 hadi shilingi 2000 kwa kadri ya matumizi ya mteja baada ya majadiliano na Kamati ya Bunge ya Bajeti.
Kabla ya majadiliano hayo tozo iliyopendekezwa katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya serikali 2022/23 ilikuwa shilingi 1,000 hadi shilingi 3,000.

Hayo yamesemwa leo Juni 2022/2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Fedha 2022.

Amesema, Serikali ilipendekeza Sheria ya Posta na Mawasiliano ya kuanzisha tozo hiyo ya shilingi 1,000 hadi 3,000 kwa ving’amuzi itakayokuwa ikitozwa kupitia malipo ya vifurushi.

“Hata, hivyo baada ya majadiliano ya kina ilionekana kwamba kiwango hicho ni kikubwa,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news