Simba SC yaanza kusafishwa kwa brashi ngumu, MO Dewji afunguka

NA GODFREY NNKO

MWEKEZAJI pekee kwa umiliki wa asilimia 49 ya hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 20 katika Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara bilionea Mohamed Dewji (Mo Dewji) amesema, wanaisafisha klabu hiyo kila sehemu inayostahili kufanyiwa hivyo.
"Tunasafisha kila sehemu ambayo inahitaji kuwekwa sawa ili turudi kwenye ubora wetu,"ameeleza Mo Dewji katika ukuta wake wa Twitter.

Ameyaeleza hayo leo Juni 3, 2022 ikiwa ni siku chache baada ya uongozi wa klabu hiyo ambayo inajivunia kufanya vema katika siku za karibuni kuanzia michuano ya ndani na ya Kimataifa kuonekana kushindwa kuonyesha makali yake.

Pia tayari Simba SC ilishatangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu, Mhispania Pablo Franco Martin (41) ikiwa ni siku 207 toka aajiriwe na klabu Novemba 6, 2021.

Pablo alifutwa kazi pamoja na Kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes ikiwa ni siku chache zimepita toka Simba SC ivuliwe Ubingwa wa Kombe la ASFC kwa kufungwa 1-0 na Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Kombe pekee alilotwaa ni Mapinduzi Cup 2022 pamoja na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Post a Comment

0 Comments