TANESCO yakoleza safari ya kutoa huduma Kidigitali jijini Mwanza

NA SHEILA KATIKULA

WANANCHI mkoani Mwanza wameshauri kutumia mfumo mpya wa kidigitali wa Ni-Konekt kuomba huduma ya nishati ya umeme.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano kwa Huduma Mteja Mkoa Mwanza,Flaviana Moshi wakati akitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa huduma hiyo. Amesema, mfumo huo unarahisha wateja kupata huduma hiyo bila kufika ofisini kwao.

"Mfumo huu ni rahisi na unaokoa muda, kwani ukijaza taarifa zako kwa usahihi siku hiyo hiyo unafungiwa umeme,"amesema.

Amesema, mfumo huo unatumia njia tatu ikiwemo kupitia Ussd, web portal na mobile App.
"Mwombaji anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA ili aweze kupata huduma ya maombi ya umeme kupitia mfumo wa Ni-Konekt.

"Mfumo huu umezinduliwa Juni 6, mwaka mpaka hivi sasa tumewaunganishia wateja wanne kwani Ni-Konekt ni huduma rahisi ambayo inarahisisha kupata umeme kwa urahisi na inapunguza urasimu na mianya ya vishoka,"amesema.
Moshi amesema mteja anaweza kutumia mfumo huo kwa simu maarufu kama kiswaswadu (kiganjani) simu janja,kompyuta,au kifaa chenye uwezo wa intaneti na kupata huduma.

"Kwa watumiaji wa Android inapatikana kwenye play store na App store kwa watumiaji wa Iphone,"amesema.
Moshi amesema, faida ya mfumo huo wa kidigitali ni kupunguza urasimu, kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa umeme,ni rahisi kufuatilia maombi na unarahisha mteja kupata huduma hiyo kwa urahisi.

"Hatua zote za huduma hiyo zitafanyika kidigitali hadi kufikia hatua ya malipo na kulipia hatimaye kupatiwa huduma stahili haraka iwezekanavyo,"amesema Moshi.

Post a Comment

0 Comments