Tembo Warriors watua Poland

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Taifa Tembo Warriors imefanikiwa kufika salama nchini Poland kushiriki mashindano ya Ulaya katika mji wa Warsaw.
Msafara huo ambao ulikuwa na wachezaji 7, Benchi la ufundi 2, Viongozi wa TAFF 2 na viongozi wa Serikali 2 ulifika Warsaw Juni 9,2022 majira saa saa moja usiku.

Kocha wa Tembo Warriors, Ivo Mapunda pamoja na wachezaji wanne wanaocheza mpira wa kulipwa Uturuki wanategemewa kufika Poland leo ili kufikia idadi ya watu 18 kwa msafara wa Tanzania.
Rais wa Shirikisho amewashukuru wadau wakuu wa safari hii ambao ni Wizara ya Michezo pamoja na Baraza la Michezo kwa kuwezesha ombi la TAFF kupitia benchi la ufundi lililotaka uwepo wa Michezo ya kimataifa ya kupima timu kabla ya kwenda kombe la Dunia.

"Kwa kweli awamu ya Sita imefany mapinduzi makubwa katika Michezo, Na hapa ni lazima tukubali kwamba Rais Samia Suluhu amekuja na maono safi katika Michezo na tunaona matunda yake kila siku. Tunamshukuru sana kwa kuendelea kuiwezesha timu yetu hasa inapoendelea kufanya maandalizi ya kushindana Kombe la Dunia,"alisema Sarungi.

Mashindano ya Poland yanatarajiwa kuanza tarehe 11 hadi 12 Juni huku Tanzania ikipangwa kuanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mwenyeji Poland.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news