TGNP wajadili mwenendo wa hali ya ukatili wilayani Msalala

NA KADAMA MALUNDE

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuangalia halisi ya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akifungua mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ulioandaliwa na TGNP.(Picha na Malunde 1blog).

Mkutano huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika kata ya Segese halmashauri ya Msalala ikiwa ni mwendelezo wa kazi ya Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoa wa Shinyanga katika halmashauri ya Msalala unaotekelezwa na TGNP kupitia Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA.

Makundi yaliyoshiriki katika mkutano huo ni Wawakilishi wa Vituo vya taarifa na maarifa kata ya Lunguya na Shilela, Idara ya afya, maafisa ustawi wa jamii, jeshi la polisi, mahakama,walimu, viongozi wa kata, watu maarufu na Wasaidizi wa Kisheria.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Joseph Mbunge akiwasilisha taarifa ya kituo hicho kwenye mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Akifungua Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga amesema licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia bado panahitajika nguvu za ziada kwa kuhakikisha kila mmoja katika jamii anashiriki kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo kutekeleza kwa vitendo Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

“Leo tumekutana katika mkutano huu kwa ajlli ya kujadili mwenendo wa ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia. Mkutano huu utasaidia kuonesha mafanikio tuliyopata tangu Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoa wa Shinyanga katika halmashauri ya Msalala unaotekelezwa na TGNP uanze mwaka 2020 na kutupatia mikakati thabiti ya kupambana na kukomesha mila kandamizi kwa wanawake na wasichana ndani ya jamii,”amesema Shija.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya, Meja Masalu akiwasilisha taarifa ya kituo hicho kwenye mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Miongoni mwa changamoto zilizoibuliwa katika mkutano ni pamoja na kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kuendelea kumalizwa kifamilia na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa kudaiwa kuwa sehemu ya wakwamishaji wa mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni kwa kuendekeza rushwa na kushiriki kumaliza kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kifamilia.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

“Kuna baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa (wenyeviti wa vijiji na vitongoji) wanakwamisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, wanatumia kesi hizi kwa maslahi yao binafsi,”amesema Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Joseph Mbunge.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Lunguya, Madulu Bujiku amesema bado kuna baadhi ya wazazi wanawashawishi watoto wafeli mitihani na
wanafunzi kukosa mahitaji muhimu ya shule hali inayosababisha kujiingiza kwenye vishawishi kwani wazazi hawawapi mahitaji ya shule watoto wao kutokana na uchumi duni wa kaya na wengine kutokuwa na kutojali tu.
Afisa Kilimo Kata ya Shilela Togolani Nkondo (Mwenyekiti wa Mkutano) akizungumza wakati akifungua mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kwa makundi ya watu wanaoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Naye Mwenyekiti wa mkutano huo, Togolani Nkondo ambaye ni Afisa Kilimo Kata ya Shilela ameiomba serikali kuingilia katia michezo ya Bahati Nasibu nyakati za kazi na kuitaka jamii kutowaruhusu watoto kucheza michezo hiyo.

“Katika suala la ulinzi wa mtoto lazima tuzuie watoto kujiingiza kwenye matendo hatarishi ikiwemo kutowaruhusu kuzurua nyakati za usiku. Na Sasa kuna baadhi ya watoto wanacheza michezo ya bahati nasibu ‘Ma bonanza hali inayohatarisha usalama wa watoto. Mabonanza haya siyo mazuri kwa wanafunzi,watoto wakatazwe,”amesema Nkondo.

Nao Wauguzi wa Vituo vya afya Lunguya na Shilela (Mwajuma Ahmad na Neema Charles) wameomba elimu zaidi iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwani kesi za matukio ya ukatili zimekuwa zikimalizwa kifamilia hivyo kukwamisha juhudi za kukomesha matukio hayo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano kuhusu Mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano kuhusu mwenendo wa hali ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia.

Msaidizi wa Kisheria Hawa Hashim kutoka kata ya Bulyanhulu amesema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wanapofuatilia kesi za ukatili wa kijinsia ni jamii kuficha matukio ya ukatili na kumaliza kesi kifamilia lakini pia wakati mwingine wamekuwa wakikwama kutekeleza majukumu kutokana na kupewa vitisho kutoka kwa wahusika wa matukio.

Post a Comment

0 Comments