'Twende kwa kasi ile ile ili zoezi hili tulimalize kwa ufanisi mkubwa,Watanzania wanatuunga mkono na wanasubiri kwa hamu zoezi hili la Sensa'

NA DIRAMAKINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa yote nchini waendelee kuongeza kasi katika uratibu wa maandalizi ya zoezi la sensa ya watu na makazi.

“Twende kwa kasi ile ile ili zoezi hili tulimalize kwa ufanisi mkubwa. Watanzania wanatuunga mkono na wanasubiri kwa hamu zoezi hili.” Sensa ya watu na makazi itafanyika Agosti 23, 2022.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Februari 18, 2022 katika kikao kazi cha viongozi wa mikoa na wilaya kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi nchini.

Post a Comment

0 Comments