Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Juni 27, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 624.08 na kuuzwa kwa shilingi 630.18 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 147.08 na kuuzwa kwa shilingi 148.38.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Juni 27, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Krona ya Sweden (SEK) inanunuliwa kwa shilingi 225.63 na kuuzwa kwa shilingi 227.82 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 144.24 na kuuzwa kwa shilingi 145.59.

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.61huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.51 na kuuzwa kwa shilingi 11.14.

Rupia ya India (INR) inanunuliwa kwa shilingi 29.28 na kuuzwa kwa shilingi 29.56 huku Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.48 na kuuzwa kwa shilingi 19.64.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2412.16 na kuuzwa kwa shilingi 2436.75 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2812.81 na kuuzwa kwa shilingi 2841.17.

Post a Comment

0 Comments