WATANZANIA TUILINDE NA KUTUNZA MISITU YETU-WAZIRI MKUU

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika utunzaji wa misitu kwa kutekeleza azma ya uhifadhi na uendelezaji misitu kwa vitendo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma, Juni 1, 2022. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

Amesema kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) imeendelea kuratibu utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji na utunzaji wa miti inayotekelezwa nchini kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Amesema hayo leo Juni 1, 2022 wakati akizindua zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma. “Watanzania tuendelee kupanda na kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa miti na misitu kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu.
Katika kipindi cha mwaka 2020/21, Halmashauri 27 kati ya 184 zilivuka lengo la kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka ambapo idadi ya miti 202,923,907 ilipandwa na miti 165,501,119 ilistawi, ambayo ni sawa na asilimia 81.6,”

Post a Comment

0 Comments