Watoto wa Mfalme wa Saudi Arabia watembelea Kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama wilayani Serengeti

NA FRESHA KINASA

WATOTO wa Mfalme wa Saudi Arabia,Salman bin Abdulaziz Al Saud wametembelea Kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama kilichopo Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kinachotoa hifadhi kwa wasichana waliokimbia aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia kutoka katika familia zao.
Kituo hicho, kinamilikiwa na Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na mapambano ya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu chini ya Mkurugenzi wake, Rhobi Samwelly.
Wamefanya ziara ya kutembelea kituo hicho leo Juni 29, 2022 ambapo wamepongeza juhudi thabiti zinazofanywa na shirika hilo katika kuhakikisha watoto wa kike linawasaidia kuwalinda na kuwaendeleza kielimu na kifani kusudi wafikie ndoto zao. 
Aidha, wameahidi kuendelea kushirikiana na shirika hilo ikiwemo kuliunga mkono kwa kulisaidia liweze kufanya vizuri zaidi katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokomeza ukeketaji, ndoa za utotoni na aina mbalimbali za ukatili. 
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama, Daniel Misoji amewashukuru kwa kufika katika kituo hicho ambapo amesema kuwa, shirika hilo kupitia kituo hicho limeendelea kuwapa hifadhi wasichana ambao hukimbia makwao kupata hifadhi kituoni hapo.

Pia limekuwa likihakikisha wanaosoma wanaendelea na masomo yao na kwa wale ambao huwa wamehitimu huwatafutia vyuo mbalimbali na kuwagharamia kusudi watimize ndoto zao na wajikwamue kiuchumi. 
Ameongeza kuwa, shirika hilo limeendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali wilayani humo ikiwa ni pamoja na Dawati la Jinsia na Watoto (Polisi), Maendeleo ya Jamii, Usatawi wa Jamii pamoja na kuwashirikisha wananchi wa makundi yote katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news