Bao la Pape Ousmane Sakho wa Simba SC latua CAF

NA DIRAMAKINI 

WINGA raia wa Senegal anayekipiga katika Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Pape Ousmane Sakho kupitia bao alilofunga dhidi ya ASEC kwenye mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika limeingia kwenye kipengele cha kuwania Bao Bora la Mwaka Afrika katika Tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Pape Ousmane Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 tu akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe katika ushindi wa 3-1 dhidi ASEC Mimosas ya Februari 13, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments