Barrick Bulyanhulu na North Mara zatwaa tuzo za TANTRADE

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya Barrick kupitia migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara imeshinda tuzo za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambazo zilikabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango, wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa STAMICO, DKt. Venance Mwesse (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano na Masuala ya ndani wa Barrick ,Neema Ndossi na Mratibu wa Uhusiano na Masuala ya Ndani wa kampuni hiyo, Abella Mutiganzi , baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt.Philip Isdory Mpango, wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam iliyofanyika jana. Barrick ilishinda tuzo za kuongoza kuuza madini katika migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara na tuzo ya mwasilishaji bora wa michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). 
Wafanyakazi wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Abella Mutiganzi (kulia) wakifurahia tuzo za ushindi baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt. Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.

Tuzo ambazo kampuni imejishindia ni kuongoza kuuza madini nje ya nchi (Export Minerals Award) kwa migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara na tuzo ya mwasilishaji bora wa michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) – (Best Employer compliance) kwa mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) , Geoffrey Meena (katikati) akiwa na Meneja Uhusiano wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Mratibu wa Uhusiano na Masuala ya Ndani, Abella Mutiganzi (kulia) baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt.Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael. Isamuhyo,(katikati) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Abella Mutiganzi (kulia) baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt. Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka makampuni yaliyoshinda tuzo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais DK.Philip Isdory Mpango, na viongozi wengine wa Serikali wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.

Barrick, imetambulika kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika mwaka wa 2021 na hivyo kuthibitisha nafasi yake kama mchangiaji mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa kijamii Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news