Waziri Mkuu ndani ya Singida siku nne

NA DIRAMAKINI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia kufanya ziara ya siku nne mkoani Singida ambapo pamoja na mambo mengine atakagua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, imeeleza kuwa Waziri Mkuu atanza ziara hiyo leo Julai 15 hadi Julai 19, mwaka huu ambapo ataanzia katika Wilaya ya Manyoni.

Akiwa katika Kata ya Solya Wilaya ya Manyoni,atapokea taarifa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida ya Solya na kuweka jiwe la msingi na baadaye kupokea taarifa ya mkoa na kisha kuzungumza na watumishi.

Aidha,Waziri Mkuu atapokea taarifa na kutembelea ujenzi wa barabara ya kilometa 10 Itigi mjini na baadaye kuzungumza na wananchi na jioni ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mtoa na kisha kuzungumza na wananchi.

Julai 16, Waziri Mkuu, atawasili Wilayani Iramba ambapo atatembelea mradi wa maji Misigiri,atazungumza na wananchi pamoja na watumishi.

Aidha, Waziri Mkuu, Majaliwa atakuwa katika Wilaya ya Makalama ambako atatembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mawe na baadaye mchana atazindua ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkalama na kusalimiana na wananchi.

Julai 18, atakuwa katika Wilaya ya Ikungi, atapokea taarifa na kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Irisya na mchana atatembelea makazi ya viongozi wa kitaifa.

Baadaye ataweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha VETA na Hospitali ya Wilaya na kuzungumza na wananchi.

Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake katika Wilaya ya Singida Julai 19, kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuzungumza na wananchi.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa na kuzungumza na watumishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news