BRELA yashiriki warsha ya 'Instaprenyua Smatsha Biashara'

NA MWANDISHI WETU

AFISA Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi.Neema Kitala (katikati), akiwasilisha mada kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA na hatua za urasimishaji wa biashara kwa wajasiriamali wa biashara za mtandaoni, katika warsha ya siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB Posta, jijini Dar es salaam. 
Katika warsha hiyo wajasiriamali hao wamepata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujikwamua ikiwa ni pamoja na urasimishaji wa biashara zao. 
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB inaenda sambamba na kauli mbiu ya "Instaprenyua Smatsha Biashara" ikiwa na lengo la kuwahamasisha wajasiriamali kurasimisha biashara zao ili kukidhi soko la ushindani.

Post a Comment

0 Comments