EWURA yateta na Wahariri, Mhandisi Lumato aeleza ruzuku ya mafuta bilioni 100/- ilivyopunguza maumivu

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 kupunguza bei za mafuta hapa nchini imeleta nafuu kubwa mitaani.
Afisa Mwandamizi Huduma kwa wateja wa EWURA, Kanda ya Mashariki, Getrude Mbiling'i akifuatilia mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Mhandisi Modestus Lumato ameyasema hayo leo Julai 16, 2022 katika kikao kazi cha siku moja na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari nchini kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

Hivi karibuni Rais Samia aliagiza ruzuku ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kukabiliana na kupanda kwa bei kuanzia mwezi Juni ili kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mhandisi Modestus Lumato (kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Julai 16,2022 jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.

"...Suala kubwa la mafuta kupanda bei ni la Dunia, lakini kila mmoja anahangaika kuona anafanyaje kwa sababu kila mmoja analia kivyake,ndiyo maana kama mnakumbuka Mheshimiwa Rais Samia amekubali kutoa ruzuku angalau kupunguza ingawa kwa macho haionekani, kwa sababu unaongeza shilingi 500, halafu yenyewe yanaongezeka shilingi 700 sasa ukiitoa huku kwa wananchi wenyewe hawaioni wanaona tena shilingi 200 imeongezeka kumbe ilikuwa imeongezeka shilingi 700," amesema Mhandisi Lumato. 

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, "Sasa,kila kukicha na sisi tunazidi kuangalia ni wapi tunaweza kusaidia kuweza kupunguza hata ninyi (wahariri) kama mna solutions au mna mawazo napenda kuyasikia mawazo yenu niyachukue kama mnafikiri ni wapi tunaweza tukasaidia katika suala hili la kupunguza bei kwenye mafuta,"ameongeza.

Gesi

Mhandisi Lumato akizungumzia kwa upande wa nishati mbadala amesema, gesi ni miongoni mwa maeneo ya vipaumbele kwa mamlaka hiyo katika kuona inatumika katika kuendeshea vyombo vya moto nchini hususani magari.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA. Titus Kaguo akizungumza kwenye kikao hicho alipokuwa akiwakaribisha wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) kwenye kikao hicho kilichofanyika leo Julai 16,2022 jijini Dar es Salaam.

"Kwenye suala la alternative fuel na kwenda kwenye gesi hili ni moja ya kazi ambayo kwa EWURA kwa mwaka huu wa bajeti tumeweka kipaumbele, kwa hiyo kama mnakumbuka hapo katikati kama wiki mbili zimepita tuliita wadau wote wanaotumia gesi, wanaozalisha gesi, wanaounganisha magari na wanaouza kwenye vituo vya kuzalishia ili kutafuta changamoto zinazosababisha watu wengi wasibadilishe magari kwenda kwenye gesi," amesema Mhandisi Lumato na kuongeza kuwa.

"Sababu kuna faida kubwa,ukitumia gesi kama ulivyosema ukitumia gesi kwa shilingi 17, 000 unaenda kilomita 300, lakini mafuta utatumia ya shilingi ngapi mpaka uende kilomita 300? Ukitumia mafuta ni kiasi kikubwa sana, lakini tulikuwa tunatafuta kwa nini watu hawabadilishi? Tumepata baadhi ya majibu mengi tu mojawapo kubwa ni elimu, elimu haijaenda kwa watu hawajaelewa faida yake. 

"Yaani wanaangalia ile hela ya kubadilishia gari ile peke yake bila kujua ile hela ya kubadilishia gari ndani ya miezi miwili au mitatu inakuwa imerudi akiwa anatumia gesi, sasa wahariri ndio sehemu yenu sasa mnatakiwa mtusaidie kuelimisha watu tukija tukawaonesha, tukawaelimisha zile hesabu zake jinsi anavyoweza kusave halafu na ninyi mkaenda kuwaambia watu watakimbia kubadilisha,"amesema Mhandisi Lumato.

"Tatizo lingine lilikuwa ni vituo, viko vichache, viko viwili tu mpaka sasa, lakini hilo nalo tumeshalitafutia solution (suluhisho) tumeruhusu wenye vituo vya mafuta waweze kuweka na vituo vya gesi pale pale na wameshapewa vibali kwa sababu mwenye jukumu hilo kubwa la kusambaza gesi kwa watu alilopewa kisheria ni TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania).

"Lakini pia TPDC ameruhusiwa kugawa hilo jukumu kwa watu wengine, kwa hiyo wengi wameshapewa Concert ya TPDC na wameshakuja kwetu (EWURA) tumewaruhusu waende wakajenge.
"Ili uwe na vile vituo vya kujazia kwenye vituo vidogo unatakiwa uwe na vituo vikubwa vya kujaza yaani kama ilivyo kwenye mafuta uwe na depo ambapo gari inakwenda inachukua kule ndio inakuja kuweka kwenye kituo kidogo, sasa vile vituo vikubwa navyo vinajengwa, TPDC anajenga kikubwa pale karibu na Mlimani City na pia kuna kampuni nyingine ya ki-Egypt (Misri) inajenga kituo kikubwa Samora,"amesema Mhandisi Lumato. 

"Hivyo vikikamilika kujengwa, vituo hivyo vikubwa. Sasa ni rahisi wengine wenye vituo vidogo vidogo kujenga zile pampu peke yake, wanakuwa wanakwenda kuchukua pale wanapeleka kwenye vituo vyao kufika mwakani tutakuwa na vituo vitatu vikubwa kuna kimoja tayari pale Pan Africa Ubungo (PanAfrican Energy) kinafanya kazi zote.

"Kwa hiyo na hivyo viwili vikija vitakuwa mother station mbili, kwa hiyo zinatosheleza kabisa watu wengine kuchukua pale na kusambaza kwingine hizo ndiyo changamoto ambazo mojawapo tulikuwa tumeziona.

"Ingawa changamoto nyingine wanasema vile vifaa bado kodi ni kubwa, kwa hiyo hilo tutalipeleka mbele nalo ili liweze kuangalia wakivitolea kodi vile watapata mauzo, kwa sababu mauzo ya gesi mwisho wa siku hela inaenda serikalini. 

"Unaweza ukasave upande huu ukapata upande mwingine, hivyo vyote tunajaribu kuangaika kutafuta solution mwananchi wa kawaida apate unafuu, na pia wa mabasi ya DART tumewashawishi watumie gesi ili nauli isije ikapanda kwa sababu wakitumia gesi hawatalalamika gharama kubwa za uendeshaji, kwa kutumia gesi gharama zitakuwa ndogo.

"Na baada ya muda wataweza kubadilisha na hata yaliyokuwepo hayo yakaanza kutumia gesi kwa sababu teknolojia zote zipo. Kwa mfano Dangote. Dangote, yale malori yake kama 600 yamebadilisha yanatumia gesi kwa hiyo ana kituo chake kule Mtwara anajaza, akijaza yakifika hapa Dar es Salaam yanaweza kuwa yamefika nusu ya ile mitungu anajaza tena Dar es Salaam anasogea anafika tena Dodoma,"amesema.

"Kwa hiyo, anakuwa amesave, amepunguza gharama kule kutoka Mtwara mpaka Dodoma ukaendesha kwa gesi tena unapokuwa umefika kule unakuwa unesave hela kwa hiyo ni selling kubwa sana. 

"Hiyo sisi tunachoomba ni elimu isambae kwa wananchi wengi, hata wenye malori ya kawaida wakiamua kubadilisha watapata faida sana badala ya kung'ang'ania mafuta ambayo hatuna control nayo, gesi tuna control kwa sababu ni ya kwetu na inatoka Songosongo hapo na hatutegemei mtu kuja kutupangia bei tunapanga wenyewe,"amefafanua kwa kina Mhandisi Lumato.

Maji

Akizungumzia kwa upande wa maji, Mhandisi Lumato amesema kuwa, "Suala la maji sisi kama EWURA tumeliangalia sana mpaka sasa hivi ukiangalia angalau kuna ahueni ukilinganisha na huko nyuma bila EWURA kwa sababu EWURA ndiye anazisimamia mamlaka zote za maji ndiye anayeenda kuzikagua na kuangalia service wanayotoa inafanana na anacholipa mwananchi? Sababu kuna wakati unakuta unalipa hewa, mita inasoma maji hayatoki.

"Sasa zile complains zote EWURA anazichukua tunamfuata mwenye mamlaka, control wewe mbona watu hawajapata maji unasoma bills (ankara) unasoma nini? Kwa hiyo control ya kwetu ndio inayofanya zile mamlaka zifanye kazi kwa bidii na zinafuatilia kwa sababu kila mmoja anaogopa ripoti yake ikitoka ni kama ripoti ya Mkaguzi Mkuu, kwa hiyo sisi ripoti yetu ikitoka tunampelekea Waziri angalia mamlaka yako inachokifanya.
"Hakuna anayependa naye ripoti yake iwe mbovu, kwa hiyo kwenye maji nao tunawafuatilia sana mamlaka zote nyingi ziko vizuri sana kwa sasa, zinajitahidi sema zina changamoto ya vyanzo vya maji. Lakini huku kwenye kusambaza kama maji yapo wanajitahidi ingawa tunawakumbusha wasiende kinyume chake,"amesema Mhandisi Lumato.

"Kwa hiyo, tunachofanya sisi ni kuwaelimisha wananchi wajue haki yao ni ipi kwa sababu maji ni haki, lakini pia wajue wajibu wao ni upi, wanatakiwa kulipa wapate maji walipe na wewe mtoa maji toa maji ili ukadai pesa.Kwa hiyo hivyo vitu wiwili lazima service nzuri na wewe uweze kupata cha kwako," amesema.

Awali, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile 
amesema, vyombo vya habari nchini vitaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi zote ikiwemo EWURA ili kuhakikisha vinafikisha taarifa mbalimbali kwa umma kwa wakati. 

"...Tuna magazeti ambayo yanafanya kazi nzuri, radio na Tv tuombe ule ushirikiano uliokuwepo unaoendelea kuwepo wa matangazo ya hapa na pale yanapopatikana kuyagawa, tukukaribishe na kwa pamoja tuone namna gani tunaijenga hii nchi yetu,"amesema Bw.Balile.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile (kushoto aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.

"Tunaomba tukukaribishe kwenye tasnia yetu...umeingia kwenye kipindi kuna dirisha zuri sana la matumizi ya gesi. Mwezi wa kwanza tuliandika habari chache sana tukiwaambia wananchi faida za gesi kwenye magari badala ya petroli, tulikuwa tuna magari kama tisa hivi, lakini wiki iliyopita tulikuwa tuna magari zaidi ya 1,000 hapa Dar es Salaam ambayo yameconvert kwenda gesi," amesema Balile.

"Ninao rafiki zangu ambao wameconvert magari ya IST wakijaza gesi ya shilingi 17,000 wanatembea kilomita 300...kwa hiyo unaweza kuona watu wameanza kuhamasika, umefika wakati mwafaka kwamba EWURA ibadili kanuni angalau kila kituo kinachouza petroli kiweze kuuza na gesi pia angalau Dar es Salaam kwa sababu miundombinu ni rahisi kuiconnect hasa kwa Dar es Salaam iwapo nia ipo," amesema Balile.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news