DC MTATIRO AAPISHWA KUWA WAKILI

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mheshimiwa Julius Mtatiro ni miongoni mwa wakili wapya 335 walioapishwa leo.
Ni katika sherehe za 66 za kupokea Mawakili wapya ambapo wameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma kuwa Mawakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama zilizopo chini yake isipokuwa Mahakama za Mwanzo.
DC Mtatiro ana shahada za juu takribani nne, ambazo ni Shahada ya Sanaa katika Elimu (BAED), Shahada ya Sheria (LLB), Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Umma (MPA), Shahada ya Uzamili ya Sera za Umma (MAPP), Stashahada ya Juu ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (PDLP), Cheti cha Juu cha Uongozi na Cheti cha Juu cha Tafsiri na Ukalimani kati ya Lugha ya Kiingereza na Kiswahili na vyeti vingine vingi.

Post a Comment

0 Comments