DCB yachangamkia fursa uchumi wa buluu Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa katika mkutano aliouandaa akiwashirikisha wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza huku wajumbe wengine wakimsikiliza katika mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya (hayupo pichani), ukiwashirikisha wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar hivi karibuni. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Rahma Ngassa akishiriki pamoja na washiriki wengine mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (hayupo pichani), ukiwashirikisha wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akipozi katika picha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (wa tatu kushoto) pamoja na wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za fedha kutoka bara na visiwani mara baada ya mkutano ulioandaliwa na Mheshimiwa Waziri kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi inayoendelea visiwani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news