FURAHIKA yafungua pazia elimu bure waliofeli darasa la saba na kidato cha nne, Serikali yatoa wito

NA DIRAMAKINI

SERIKALI imesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya nchi itaendelea kuwajengea uwezo vijana ambao wamekosa fursa au sifa za kuendelea na masomo ili waweze kujiendeleza kupitia vipaji walivyo navyo nchini.
Hayo yamesemwa Julai 15, 2022 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Mwanahamis Adam Ameir ambaye alimwakilisha Waziri Leila Muhamed Musa katika uzinduzi wa mradi wa huduma ya afya wa kujitolea kwa mama na mtoto.

Sambamba na kuwatunuku vyeti wanafunzi ambao wamemaliza katika mradi huo unaondeshwa na Chuo cha Furahika (Furahika Education College Tanzania) kilichopo Buguruni jijini Dar es Saalam."Tumekuja hapa kwa ajili ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wetu ambao wanamaliza katika huu mradi wetu wa Furahika ambao wamepata mafunzo mbalimbali ya udereva unesi pamoja na ualimu tuko katika kushirikiana nao.

"Awali kulikuwa na jiwe la msingi ambalo limewekwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Leila Muhamed Mussa.Furahika tunafanya kazi pamoja kupitia Wizara ya Elimu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Ni kupitia msaada ambao unatoka katika Shirika la Ujerumani kwa hiyo vijana wote wa Tanzania Bara na wa Zanzibar pamoja wanajumuika hapa kupewa mafunzo haya. Ni vijana ambao wamekosa fursa na nafasi ya kuendelea na masomo sifa zao haziwaruhusu kuendelea na vyuo ambavyo vipo vya elimu ya juu, kwa hiyo hapa wanapata mafunzo bure kabisa wakiwa na sifa zao za chini kabisa. 

"Wanapata mafunzo ya udereva, unesi na ualim, elimu ambayo inawasaidia wao kuwa na sehemu ya kuanzia katina maisha yao.
"Maana yake ukiwa hauna ujuzi wowote huna maarifa yoyote huna popote pa kuanzia, lakini wakiwa tayari wamepatiwa mafunzo mana yake wana sehemu yoyote ya kuanzia. Ukiwa na mafunzo yako ya udereva unaweza kujiajiri kuomba kwenye taasisi, watu binafsi, unaweza hata mwenyewe maarifa yale ukayatumia yanaweza kukusaidia,"amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Ameendelea kusisitiza kuwa, "Kwa hiyo kama wazee, wananchi tunatakiwa kuunga mkono hiki chuo ili kuwahusisha vijana mbalimbali kutumia hizo fursa na mafunzo ambayo yanatolewa bure, wazee wajitolee wanachangia ada ndogondogo tu kusaidia watoto wao kufanya mafunzo ya vitu na vifaa ambavyo vinahitajika kufanya mafunzo ya vitendo na masuala mengine,"amesema.

Mkuu wa Chuo

Naye Mkuu wa Chuo cha Furahika Education College Tanzania, Bw. David Msuya amesema kuwa, mradi huo una thamani ya shilingi milioni 400 huku ukiwa ni wa miaka mitano.
"Tunazindua mradi huu wa kujitolea wa huduma ya mama na mtoto, mradi huu una thamani ya shilingi milioni 400 na ni wa miaka mitano kwa lengo moja la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi. 

"Kama unavyoona pale mwakilishi wa Mheshimiwa Waziri, Naibu Katibu Mkuu yupo ambaye alikiwa mgeni rasmi wetu, lakini pia unaona Mkurugenzi wa Elimu wa Wizara Zanzibar yupo.
"Msingi Mkuu wa Mradi huu ni kuwafikia vijana wengi kuwapa mafunzo ya afya, lakini wakajitolee kwenye hospitali za vijijini kusapoti juhudi za serikali sio lazima wote waajiriwe kuna watu wanaguswa mioyoni wapete ujuzi wa mafunzo ya afya wakajitolee kwenye hospitali za serikali vijijini tu sio mjini.

"Mjini hawawezi kupata mtu wa kujitolea, lakini pia wale watawahudumia wagonjwa mbalimbali wa kisukari, HIV, huko vijijini kupitia mitaa wengine watakuwa waelimisha rika kwa hiyo huo ndio msingi wetu.
"Mradi huu tunashirikiana na Wizara ya Afya Tanzania na kule Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu ambapo wanafunzi unaowaona hapa robo tatu yao waliopo hapa wameletwa kutoka Zanzibar kupata mafunzo na leo tunawaaga bure bila kulipa chochote. Tunaipongeza Serikali ya Rais Mama Samia na Serikali ya Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kazi kubwa wanayofanya kutambua elimu ni kitu gani," amesema Msuya.

"Tunachukua wanafunzi waliofeli darasa la saba, kidato cha nne, kufeli darasa la saba sio mwisho wa mafanikio, kufeli kidato cha nne sio mwisho wa ndoto zao. Sisi tunataka hawa wayafikie mafanikio, wafikie ndoto zao free of charge. 

"Kama mnavyojua vyuo ni gharama, lakini sisi tunafanya hivi kupitia wafadhili wetu Wajerumani wanatutaka tufanye hivi. Ndio maana tunazindua mradi ule wa huduma ya mama na mtoto chuo hiki kinamilikiwa na shirika kwa hiyo tuna mtandao pia wa ajira.

'"Sehemu ya pili tumejipanga kushirikiana na Serikali kutoa elimu nzuri kwa ajili ya kila mtoto ayafikie malengo yake. Kama tulivyojipanga unaweza kuona Dar es Salaam tunaongoza sisi kwenye masuala ya Hotel Management, ufundi wa kushona, udereva, tuko vizuri sana, sina mtoto anayezurura mtaani tukiwapeleka field wengine wanatakiwa huko huko.
"Tunaendesha kozi zetu za certificate wengine wanasoma kozi fupi ndo sifa yetu ya usajili wetu tunatoa certificate. Haturuhusiwi kutoa diploma kwa hiyo usajili wetu ni certificate sio diploma, lakini tuna mtandao wa fursa ya ajira kwa kila mwanafunzi anayesoma FURAHIKA EDUCATION COLLEGE TANZANIA anaposoma anasoma chuo sahihi chenye mafanikio kinachotambulika na kuheshimika na Serikali.

"Wito wetu ni kwamba wazazi pamoja na kwamba tunatoa elimu bure bado wazazi wanakuwa wanarudi nyuma kwa sababu mwanafunzi anapokuja chuoni tunamwambia nunua uniform (sare) sisi ada hatuchukui vifaa vile kiatu uniform nunua, lakini mzazi anataka mfadhili alipie na shati la kuvaa mwanafunzi hiyo kidogo inakuwa changamoto, lakini sisi tunawataka wazazi watuletee watoto kwa sababu shule ya msingi wanavaa uniform chuo lazima wavae.
"Sisi tuko chini ya NACTVET kwa hiyo tuna taratibu zetu uniform ni kitu muhimu sana kwa mwanachuo ni hivyo tu anavyogharimia vifaa vyake vya darasani, lakini sasa hivyo navyo mzazi anaona ni gharama anataka chuo kimgharimie yaani mfadhili analipia ada shilingi milioni moja kwa short course sasa mzazi anataka tumlipie na shati. Tuwaombe wazazi wasiwaache watoto wa kike nyumbani wakapata mimba zisizotarajiwa wawalete masomoni ili wafikie ndoto zao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya Mama Samia.
"Ndio maana Mheshimiwa Rais amesema hata waliozaa kama walipata alama nzuri walizaa kwa bahati mbaya wapelekwe sekondari wakaendelee na masomo yao hata sisi tunasema kama ulifeli bila tu mimba hata kama ulipata mimba njoo usome FURAHIKA upate ujuzi kwa feature yako ya wakati ujao,"amefafanua Msuya.
 

FURAHIKA EDUCATION COLLEGE TANZANIA

Chuo kinakaribisha wanafunzi kusoma bure, lengo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan ya Elimu bure, hivyo mashirika na watu mbalimbali wanakaribishwa kuleta wanafunzi na taasisi ama mashirika yenye namna ya kusaidia taasisi hii wanakaribishwa pia, ili kuwanuia watoto wa kike kupata elimu iliyo bora.

 

 KOZI ZINAZOTOLEWA

Ufundi Umeme

Ushonaji

Kompyuta

Udereva

Upambaji

Kilimo

Marketing Officer

Poker meet digital, Secretary courses, Ufugaji wa Samaki, Elimu ya Mazingira,  Ualimu wa Chekechea,  Makeup.  Ushonaji , Compyuta, Upambaji na Ususi, Hotel Management, English Course, Social workout guiding, Masijala, Ufugaji wa Kuku, Taxation.

Post a Comment

0 Comments