Haji Manara afungiwa miaka miwili, faini milioni 20/- kwa kumvujia heshima Rais wa TFF

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Julai 21, 2022 imetoa maamuzi kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga, Haji Manara.

Kamati ya Maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na faini ya sh. milioni 20 kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF, Wallace Karia

Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

Post a Comment

0 Comments