IJP Wambura:Tupo tayari kupokea marais wa EAC jijini Arusha

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camilius Wambura amewaomba wananchi hususani wakazi wa Jiji la Arusha kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na wale wote wenye nia ya kuchafua taswira nzuri ya nchi na jiji la Arusha.
IJP Wambura amesema Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha amani na utulivu unakuwa wa kutosha ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wanaofika nchini Tanzania.
Amesema hayo leo Julai 21 2022 jijini Arusha wakati akitoa taarifa juu ya ujio wa Marais wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao watafanya mkutano huo jijini Arusha siku ya tarehe 22 Julai 2022.

Post a Comment

0 Comments