Hizi hapa bei mpya za mafuta kuanzia leo Julai 6, 2022 Tanzania Bara

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zimeanza kutumika kuanzia leo Jumatano ya Julai 6,2022 saa 6:01 usiku. 
Kwa mujibu wa EWURA,Katika kukabiliana na ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, Serikali imetoa ruzuku nyingine ya Shilingi billioni 100 kwa mwezi Julai 2022. 

Ruzuku imeelekezwa katika mafuta ya petroli na dizeli kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1. Kiasi kikubwa cha ruzuku kimeelekezwa katika mafuta ya dizeli kwa lengo la kudhibiti mfumuko wa bei (inflation) kwa sababu dizeli hutumika zaidi katika shughuli za kiuchumi ikiwemo katika uzalishaji viwandani na katika usafirishaji wa mazao na bidhaa nyingine;


Post a Comment

0 Comments