Kidunda amdunda Katompa ang'ara WBF

NA DIRAMAKINI

BONDIA Mtanzania kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Seleman Kidunda amefanikiwa kumchapa kwa ushindi wa majaji wote watatu mpinzani wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Erick Tshimanga Katompa katika pambano la ubingwa wa WBF lililofanyika uwanja wa Majimaji Songea mkoani Ruvuma.
Kidunda baada ya kushuka dimbani aliwashukuru watanzania na mashabiki wa ngumi kwa sapoti yao licha ya mpinzani wake kuwa bondia mzuri  alihakikisha anaibuka na ushindi nyumbani.

Naye Katompa amesema,mchezo ulikuwa mzuri licha ya kupoteza pambano hilo dhidi ya mpinzani wake Kidunda.

Wakati huo huo, bondia mwenye mikwara mingi Karimu Mandonga alipata kipigo cha TKO kutoka kwa Shabani Kaonekana raundi ya tatu.

Mabondia wengine walioshinda ni Ismail Galiano ambaye alimtwanga KO, Buda Chikoko kutoka Malawi, George Bonabucha akimtandika kwa TKO, Yusuph Alli.

Aidha, Ezra Paul amefanikiwa kumchpa kwa KO ya raundi ya kwanza, Kasim Gambo, Grace Mwakamele amemtandika Suzana Mahenge kwa TKO, Khalid Chokoraa ameambulia sare dhidi ya Chidi Benga huku Musa Chitepete akimchapa Salvatory Urio kwa pointi.

Post a Comment

0 Comments