Kinana awasili Katavi kwa ziara ya kikazi

NA SAID MWISHEHE

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi itakayokwenda sambambamba na kupokea taarifa na kukagua miradi ya maendeleo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akiwa katika picha mbalimbali akisaliamia na wana CCM mkoa wa Katavi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi sambamba na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI.

Katika ziara hiyo ya kikazi ameongazana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka na baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Katavi Kinana amepokelewa na Wana CCM Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Beda Katani.

Baada ya kuwasili Kinana akiwa na Shaka wamepata nafasi ya kusailiamana na wanachama wa Chama hicho na kisha kupokea taarifa ya CCM na Serikali Mkoa wa Katavi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahaman Kinana akisailimiana na viongozi wa Chama na Serikali mkoa wa Katavi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda kwa ajil ya kuanza ziara mkoani humo.

Akipokea taarifa hiyo Kinana ameelezwa hali ya mwenendo wa Chama na Serikali na kwa sehemu kubwa ameambiwa hali ni shwari na kwamba viongozi wamekuwa na ushirikiano mkubwa hali inayofanywa utekelezaji wa Ilani kufanyika kwa kiwango cha kuridhisha.

Kwa mujibu wa ratiba Kinana ambaye ameanza ziara leo Julai 25 ,2022 akiwa mkoani hapa mbali ya kupokea taarifa ya Chama na Serikali atazindua mradi wa fremu 15 za biashara, pia atatembelea mradi wa fremu za vibanda 188.
Matukio mbalimbali katika picha baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya kikazi.Aidha Kinana atazindua kituo cha afya na kuzungumza na wananchi na wanachama, pia baadae atazungumza na WanaCCM na viongozi mbalimbali . Kinana atakuwa katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu ukiwemo Mkoa wa Katavi na kisha kuelekea Mkoa Rukwa, Songwe na Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news