Maandalizi ya Sensa Agosti 2022 yashika kasi, makatibu wakuu wakutana Dar


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.
Mtakwimu Mkuu Zanzibar Bw. Salum Kassim Ali akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Makatibu Wakuu wakifuatilia kikao hicho, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi , katikati ni Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean. Ndumbaro.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean. Ndumbaro akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akichangia jambo wakati wa kikao cha kujadili maandalizi ya masuala ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean. Ndumbaro.
Mshauri Mwelekezi wa TEHAMA Sensa Bw. Steven Lwendo akiwasilisha taarifa wakati kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishwaji wa mada.
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Manunuzi na Ugavi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Hirtrudice Jisenge akichangia jambo wakati wa kikao hicho. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Post a Comment

0 Comments