'Mageuzi makubwa ya kilimo ndio yatakayowainua wananchi Kibakwe'

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amehimiza watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kufanya mageuzi makubwa ya kilimo kwa kuwekeza katika miradi ya kimkakati iltakayoongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Wananchi wakimsikilza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kikuyu Kata ya Ipera Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Lazima tuwekeze fedha kwenye miundo mbinu ya uzalishaji wa kilimo, wataalam wa kilimo wanaojengewa uwezo na Wizara ya Kilimo, wafanye kilimo shambani nawatumie maarifa waliyopata kwa kushirikisha wakulima,”amesema. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kirusi jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene wakati alipofanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinusi Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Kata ya Malolo na Kata ya Ipera ni eneo ambalo limejikita katika kilimo cha umwagiliaji, halmashauri itizame namna ya kuimarisha miundo mbinu ya maji ili maji yasipote alisema Waziri,”amesema.
"Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, katika bajeti yake ya 2022-2023 imejikita katika maeneo ya uzalishaji, bajeti ya kilimo imeongezwa kutoka bilioni 200 mpaka bilioni 900, hivyo fedha nyingi zitaletwa kijijini katika miradi ya kimkakati ya kilimo,"amesema. 

Amefafanua kuwa, Serikali imeleta pembejeo za ruzuku, baadhi ya gharama zitalipwa na serikali ili mwananchi wapate pembejeo kwa bei nafuu ni lazima maafisa kilimo wajue hiyo mifumo ili waweze kuwasaidia wakulima.

Awali Diwani wa Kata ya Ipera, Mhe. Festo Myuguye ameomba serikali kupimia wananchi maeneo yao na viwanja vyao, ili wananchi waweze kupata fursa ya kutumia hati za viwanja vyao kupata mikopo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi katika Kituo cha afya Ipera kilichotengewa na Serikali shilingi milioni 500 katilka jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa. 

“Tunaomba pia Serikali itusaidie kujenga miundombinu ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo ili kuwafikia watu wengi, miundombinu iliyopo ilijengwa kabla ya kijiji kuwa kikubwa,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news