Mama Mariam Mwinyi aipongeza CRJE kwa kuunga mkono maendeleo Zanzibar

NA DIRAMAKINI

MKE wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi ametoa pongezi kwa Kampuni ya ujenzi ya CRJE ya nchini China kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwawezesha wanawake wakiwemo wakulima wa mwani.

Mke wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akizungumza na ujumbe wa Kampuni ya CRJE, walipofika katika ofisi za taasisi hiyo Migombani Unguja kwa ajili ya kukabidhi msaada wa vifaa vya utengenezaji wa sabuni ya mwani kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa bidhaa za mwazi Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo huko ofisini kwake Ikulu ndogo Migombani, Zanzibar wakati alipokutana na uongozi wa Kampuni ya ujenzi ya CRJE ya nchini China.

Katika mazungumzo yake, Mama Mariam Mwinyi ametoa pongezi kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwasaidia katika kunyanyua hali za maisha za wanawake na Wazanzibari kwa ujumla.

Amesema kwamba, hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasadiia akina mama wanaolima mwani kwa kuwaweka salama kutokana na kutoa misaada kadhaa ikiwemo vifaa vya kulimia mwani, viatu, glavu, dawa za kuchanganya sabuni, mabeseni kwa ajili ya matumizi ya kutengezea sabuni pamoja na vifaa vya sabuni.

Sambamba na hayo, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya ‘Zanzibar Maisha Bora Foundation’ (ZMBF), alieleza haja kwa uongozi wa kampuni hiyo ya kusaidia zaidi kwa lengo la kuwaongezea uwezo wanawake katika kilimo cha mwani.

Ameongeza kuwa, akina mama wanaolima mwani wanahitaji vitu katika kufanikishwa katika wanavyovifanya na hivi sasa kinachozingatiwa zaidi hivi sasa ni kuongeza ubora katika bidhaa zao.

Naye Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya CRJE ya nchini China, Yussuf Fabian Saimon, alitoa shukurani kwa Mama Mariam Mwinyi kwa ukaribisho wake na kusema kwamba CRJE hapa Zanzibar imeanza tokea mwaka 2003 huku akieleza majengo kadhaa yaliyojengwa hapa Zanzibar na Kampuni hiyo.

Katika maelezo yake Meneja huyo alisema kwamba kwa vile kampuni yake inafanya kazi na Serikali imeona ni vyema kile wanachokipata watoe msaada wao kwa Serikali na wananchi kwa ujumla wakiwemo wakulima wa mwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news