Mwinjilisti Temba ataja mambo matatu kuhusu Bandari Kavu Kwala

NA DIRAMAKINI

MUHUBIRI na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Redio Penuel ya Marangu mkoani Kilimanjaro amesema kuwa, ili kuongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam kuna umuhimu mkubwa wa kuharakisha Bandari Kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani.
"Awali ya yote nimpongeze sana Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya kwa ajili ya kuwezesha ustawi bora wa uchumi wa Watanzania na Taifa kwa ujumla.

"Tumeona namna ambavyo anapambana kuhakikisha uanzishwaji na uendelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo unafanyika, mijini na vijijini. Hii ni ishara na hatua njema sana. Nichukue nafasi hii kumuomba Mheshimiwa Rais mamá yetu Samia akafungue Bandari kavu ya Kwala mizigo yote ipitilize mpaka Kwala;

Mwinjilisti Temba ameyasema hayo leo Julai 5, 2022 wakati akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuifungua Bandari Kavu ya Kwala ili kuongeza ufanisi na kuimarisha mapato kulingana na mizigo inayotoka na kuingia katika Bandari ya Dar es Salaam. 

Amesema, hatua hiyo ikifikiwa, itawezesha Bandari ya Dar es Salaam kuwa ni eneo la rekodi tu ya mizigo yote na Kwala eneo la kutoa mizigo,hatua ambayo itaongeza udhibiti, kukabili wizi na udanganyifu ambao umekuwa changamoto kubwa.

Jambo la pili, Mwinjilisti Temba amesema kuwa, Shirika la Reli Tanzania (TRC) litapata pesa za kujikimu kwa kuwa litabeba mizigo yote na Kwala gharama za kutunza mizigo zitakuwa chini kutokana na gharama za aridhi huko na ukubwa wa eneo. 

Akizungumzia jambo la tatu, Mwinjilisti Temba amesema kuwa, hatua hiyo itapunguza msongamano jijini uliofikia upotevu wa mabilioni ya fedha kwa siku.

Pia amesema, hatua hiyo itawezesha ukuwaji uchumi na vijana zaidi ya laki tatu watapata ajira kwa malori zaidi ya elfu 20 ya mizigo yatayoishia Kwala hadi Chalinze ambapo yadi, hoteli.maduka na kadhalika yatakavyofunguliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news