NBS yataja sababu za mfumuko wa bei kuongezeka mwezi Juni

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa, mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 umeongezeka hadi asilimia 4.4 kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2022.
"Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2022.

"Kuongezeja kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Mei, 2022;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news