OR-TAMISEMI yatangaza habari njema Temeke huku ikitoa maagizo

NA OR TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkandarasi Group Six Internation Ltd kuhakisha ifikapo Septemba 30 kuhakikisha amekamilisha miradi ya ujenzi wa bababara ya Nzasa Kilungule-Bunza yenye urefu wa kilomita 7.6 na ujenzi wa kituo cha daladala katika eneo la ekari tano.
Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Julai 8, 2022 wakati akikagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha miradi hiyo yote inayogharimu shilingi bilioni 21.5

Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 20, ujenzi wa makaravati sita na ujenzi wa kituo cha daladala cha kuhudumia Coaster 100 kwa wakati mmoja, maduka 114, mini supernaket tatu, mgahawa, huduma za benki na vyoo.
Pia, mkataba huo umeongezewa kazi za ujenzi wa soko la Zakhem lenye ukubwa wa mita za mraba 4,750 ambalo limesanifiwa kuwa na vizimba 136, maduka 150, vibanda vya kuku 35, vyoo 9 na ujenzi wa maegesho ya magari yasiyozidi 25 kwa wakati mmoja.

Bashungwa amesema, kutokana na changamoto ambazo tayari zote zimetatuliwa, mkataba wa awali ulitakiwa kukamilika Juni 2021, lakini kutoka na changamoto za umiliki wa ardhi, kuchelewa kumlipa mkandalasi kwa kazi alizokamisha na mradi kupita kwenye hifadhi ya bomba la TAZAMA imepelekea mkandarasi kuongezewa muda.
Aidha,ametoa siku 14 kwa Mkurungezi wa Halmashauri ya Temeke kulipa fidia ya nyumba tatu kwenye makutano ya barabara ya Mbande ili barabara iwe na upana ili madereva waweze kuonana kwenye makutano ya barabara ya Nzasa, Kilungule na Mbande.

Bashungwa amesema, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tayari ametoa fedha zote za miradi hiyo kwa hiyo mkandarasi anatakiwa kufanya kazi kwa ubora na viwango na kuhakikisha miradi inakamilika ndani ya muda kufikia Septemba 30 ili wanannchi waanze kupata huduma.
Naye Meneja wa TARURA Temeke, Mhandisi Paul Mhere amesema mradi umekamilika kwa asilimia 75 ambayo ni barabara ya Nzasa-Kilungule-Buza yenye urefu wa kilomita 5.4 za lami na kilomita 2.2 za zege zitajumuisha mifereji ya pembeni, njia za wanaoenda kwa miguu na taa za barabarani.

Pia daraja moja lenye urefu wa mita 20 linalounganisha Kata ya Kilungule na Buza ambalo tayari limeshakamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news