PURA:Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika kuongeza ajira 10,000

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Halfan Halfan amesema kuwa mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) wa mkoani Lindi utasaidia kuongeza ajira kwa watanzania ambapo kutakuwa na ajira za watu takribani 10,000.
Halfan ameyabainisha hayo alipotembelea Banda la PURA katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 46 yanayoendelea Katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam amesema Serikali imeonesha nia ya kuwanufaisha wazawa katika mradi huo.

Amesema, katika mradi huo watahitajika wafanyakazi takribani 500, na kwamba eneo lile kutakuwa na ajira nyingi kwa watu wa bodaboda na mama ntiliye na wajasiriamali wengine.
"Mradi huu utakuwa na tija kwa taifa kwanza ule mradi utadumu kwa zaidi ya miaka 50 ukitoa tija pili gesi hiyo itauzwa nje ya nchi tutapata pesa za kigeni tatu gesi, hivyo itatusidia kufanya uzalishaji wa ndani,”amesema Halfani.

Kwa upande wake Mfanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi cha Mafuta na Gesi (OGAOGA), Frank Mwankesi ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira wezesha ya ajira katika sekta ya madini na gesi.

Amesema, Serikali imezigawa mamlaka ya uchimbaji wa mafuta na gesi kwenye madaraja mawili ya uchimbaji lile la chini na lile la juu.

"Naipongeza na kuishukuru serikali kwa kuweka watu makini na kuwasikiliza Watanzania hasa kwa wakati huu wa uhaba wa ajira,”amesema Mwankesi.

Tumaini Abdallah mmmoja wa vijana wanaofanya kazi kwenye Kampuni za kizalendo zilizonufaika na mradi wa LNG, ametoa shukrani kwa PURA kwa kuziamini kampuni za ndani za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo wamepata kuaminika kwa kampuni za kigeni zinzokuja kutekeleza uchimbaji wa gesi asilia mkoani Lindi.

Aidha, alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kujitokeza kwa wingi kwenye fursa hiyo kwa kuwa serikali ipo tayari kuwapa nafasi.

“Vijana msiogope msaada upo na serikai ipo kwa ajiri yetu kama ambavyo sisi tumenufaika kwenye radi huu,"amesema. 

Post a Comment

0 Comments