Rais Dkt.Mwinyi ateta na Mkuu wa Majeshi, ampongeza

NA DIRAMAKINI 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,Jenerali Jacob John Mkunda aliyefika Ikulu kujitambulisha na kumpongeza kwa dhati kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda wakati alipofika Ikulu jijini Zanzibar na Ujumbe wake kujitambulisha Julai 14, 2022. (Picha na Ikulu). 

Dkt.Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu kumfanyia wepesi kiongozi huyo katika utekelezaji wa kazi zake, huku akibainisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupata kiongozi sahihi mwenye uwezo wa kulisogeza mbele kutoka hapo lilipo. 

Amemuahidi ushirikiano kiongozi huyo, hususan katika utatuzi wa changamoto zitakazojitokeza katika utendaji wake, huku akionesha imani kubwa kwake kwa kuwa na weledi na uwezo mkubwa. 

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,Jenerali Jacob John Mkunda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kumpandisha cheo na hatimaye kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, sambamba na Uteuzi wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman.

Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza mtangulizi wake Jenerali Mabeyo kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuliimarisha jeshi hilo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news