Yanga SC yaachia 'nusu bilioni' kupata saini ya Stephane Aziz KI leo usiku

NA DIRAMAKINI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC ambao wana maskani yake maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam wameendelea kufanya usajili wa aina yake ili kujiimarisha.
Usajili huo ambao unajumuisha nyota mbalimbali wa ndani na nje, leo usiku wa kuamkia Julai 15, 2022 wamemtambulisha nyota na kiungo mshambuliaji kutoka Afrika Magharibi, Stephane Aziz KI kama mchezaji mpya.

Aziz Ki amenunuliwa kwa dau ambalo linatajwa kuvunja rekodi kwa timu ya ndani kununua mchezaji huyo. 

Inatajwa kuwa, karibia nusu bilioni imetumika kuipata saini ya nyota huyo ambaye ni tegemezi katika timu ya Taifa ya Burkinafaso.

Post a Comment

0 Comments