Rais Dkt.Mwinyi awaandalia chakula, zawadi maalumu wanafunzi waliofaulu vizuri mitihani ya Taifa

Baadhi ya wanafunzi wa skuli za sekondari Pemba waliofaulu vizuri mitihani yao ya Taifa wakipata chakula maalumu kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba leo Julai 29,2022, wakati wa hafla ya kuwapongeza.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita na nne waliofanya vizuri mitihani yao ya Taifa wakati wa chakula maalumu na kuwakabidhi zawadi,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba Pemba leo.Kulia ni mkewe wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na kushoto kwa Rais ni mfanyabiashara maarufu Zanzibar, Bopar.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe mama Mariam Mwinyi akimpongeza mwanafuzi wa kidato cha nne wa Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro Pemba,Kassim Khamis Omar, kwa kufaulu vizuri mtihani wake wa Taifa,wakati wa chakula maalumu na kuzawadiwa zawadi wanafunzi waliofaulu vizuri mitihani yao, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba leo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya kompyuta mpakato mwanafunzi Abdulhalim Rajab Ame wa kidato cha nne kutoka Skuli ya Fidel Castro Pemba,wakati wa chakula maalumu alichowaandalia na kuwapongeza kwa kufaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba leo.
Wanafunzi wa skuli mbalimbali za Sekondari Pemba wa Kidato cha Sita na cha Nne, waliofanya vizuri mitihani yao ya Taifa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi na kujumuika nao katika chakula cha mchana kilichofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita na cha nne Pemba kwa kufaulu vizuri mitihani yao ya Taifa, wakati wa chakula maalumu alichowaandalia na kuwakabidhi zawadi katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Wilaya ya Chake Chake Pemba leo. Wanafunzi wa kidato cha nne na sita Pemba wakishangilia wakati wa kukabidhiwa zawadi kwa ufaulu wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Pagali Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news