Rais Dkt.Mwinyi awaeleza jambo wafugaji wa samaki

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea mabwawa ya kufugia samaki huko Kibaridi Pujini, Pemba na kuwaeleza wafugaji wa samaki kwamba serikali itachukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha wanapatiwa vifaranga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akivua samaki katika bwawa la kufugia samaki la Kikundi cha Milk Fish Farm Pujini Kibaridi, alipotembelea mradi huo, akiwa katika ziara yake kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kusini Pemba.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo Julai 27, 2022 wakati akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya kitaalamu ya ufugaji wa samaki kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Milk Fish Farm Pujini Kibaridi. Bw, Ahmed Salum Issa wakati akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Mabwawa ya Kufugia Samaki ya Kikundi cha Ushirika cha Milk Fish Farm Pujini Kibaridi Wilaya ya Chakechake Pemba huku akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika huo, Bw. Ahmed Salum Issa kushoto wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Post a Comment

0 Comments