Rais Dkt.Mwinyi:Amani, umoja na mshikamo uliopo nchini ni nguzo muhimu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameeleza matarajio yake kwamba mafanikio zaidi yataendelea kupatikana kutokana na amani, umoja na mshikamo wa wananchi uliopo hivi sasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Munawwara Mfikiwa Wilaya ya Chakechake Pemba leo.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo mara baada ya kujumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa huko Masjid Murawwar, Mfikiwa, Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika maelezo yake, Alhaj Dkt. Mwinyi amesema kwamba, ana imani kubwa baada ya miaka mitano ijayo mafanikio makubwa yatapatikana kutokana na ushirikiano, umoja na mshikamano mkubwa uliopo ambao ameuona wakati wa ziara yake katika mikoa yote ya Unguja na Pemba.

Alhaj Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa kuendeleza hatua hiyo ambayo inaleta mwanga wa matumaini na maendeleo makubwa kwa Zanzibar.

Hivyo, Alhaj Dkt. Mwinyi amesisitiza haja kwa kila mwananchi kuwajibika katika sehemu yake ya kazi ili Zanzibar iweze kupata maendeleo zaidi.

Alhaj Dkt. Mwinyi amesema kuwa, katika ziara yake yote aliyoifanya Unguja na Pemba amegundua ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wananchi sambamba na amani, utulivu na mshikamano uliopo.

Pia, Alhaj Dkt. Mwinyi almeipongeza Taasisi ya Milele Foundation kwa juhudi zake za kuiunga mkono Serikali katika kusaidia miradi kadhaa ya maendeleo pamoja na huduma za kijamii.
Ameipongeza taasisi hiyo ambayo imejenga msikiti huo kwa hatua zake za kuendelea kutoa huduma za msikiti huo mpya ambao ulizinduliwa mnamo Disemba 24, 2021 na Waziri Haroun Ali Suleima kwa niaba ya Alhaj Dkt. Mwinyi.

Aidha, Ahaj Dk.t Mwinyi amelikubali ombi la kuwa mlezi wa msikiti huo ambao alisifu ujenzi wake ambao unatoa hamu na ari kwa waumini kwenda kufanya ibada wakati wote kutokana na uzuri wake.
Mapema akitoa hotuba ya Sala ya Ijumaa, Sheikh Khalifa Mrisho Omar alitoa pongezi kwa Rais Dkt.Mwinyi kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.

Sambamba na hayo, alisisitiza haja kwa walezi na wazazi kuwalea watoto wao vyema na kuwafundisha maadili yaliyo mema.

Naye Meneja wa Milele Foundation, Abdullah Said Abdallah alimuhakikishia Alhaj Dkt. Mwinyi kwamba taasisi hiyo itaendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt.Mwinyi ili kuwasogezea huduma wananchi.
Alieleza kwamba, kamati ya msikiti huo pamoja na waumini wote wa Mfikiwa wataendelea kumuombea dua Alhaj Dkt. Mwinyi ili aweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news