Rais Samia aomboleza kifo cha msanii Bi Hindu

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa,amepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha msanii maarufu wa Kaole, Bi.Chuma Selemani (Bi Hindu).
Mheshimiwa Rais ameyasema hayo kupitia taarifa fupi aliyoitoa leo Julai 9, 2022 huku akitoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo.

"Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii maarufu wa Kaole, Chuma Selemani maarufu 'Bi Hindu'. Uweledi wake wa uigizaji na matumizi ya lugha ya Kiswahili yalileta mvuto kwa watazamaji wa Rika zote. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amin,"amesema Mheshimiwa Rais Samia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa awali na mjukuu wake alisema kuwa, bibi yake alifariki akiwa nyumbani kwake Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alisema, Bi Hindu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu hadi umauti ulipomkuta.Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.

Post a Comment

0 Comments